Na Erick Dilli-Dodoma
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) inashiriki katika wiki ya afya kitaifa 2025 inayofanyika jijini Dodoma ambapo wananchi watapa huduma za matibabu ya kibingwa ya mifupa, ubongo, mgongo, mishipa ya fahamu na ushauri wa kitaalam.
Uzinduzi wa wiki hiyo umefanyika leo Ijumaa 04, Aprili katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Conventional Center Jijini Dodoma ambapo Mdahalo maalam unafanyika pamoja na utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi
Afisa Muuguzi kutoka MOI Bi. Magreth Kumpuni amesema wanachi watakaotembelea banda la MOI watapata fursa ya matibabu ya kibingwa ya mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu
“Tunatoa ushauri kuhusu huduma za kibingwa za Mifupa, Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu pamoja na maswala ya magonjwa ya ndani na mazoezi tiba”amesema Bi. Magreth na kuongezea
“Watalaam wapo wa kutosha wabobezi na tupo tayari kutoa huduma bora kwa wakazi wa Dodoma”
Wiki ya afya kitaifa 2025 imeanza leo April 04 na kutamati April 08, 2025 ambapo ushauri na elimu utatolewa bure.