Na Amani Nsello- MOI
Matibabu ya ugonjwa wa kiharusi yanatarajiwa kuimarishwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kufuatia makubaliano ya ushirikiano baina ya Taasisi ya Umahiri ya Matibabu ya magonjwa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu ya Barrow kutoka Arizona nchini Marekani.
Hayo yalibainishwa Julai 01, 2025 na Prof. Michael Lawton, Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Barrow wakati wa ziara yake ya kikazi katika Taasisi ya MOI.
Prof. Lawton alisema dhumuni la kushirikiana na MOI katika mafunzo na tafiti pamoja na kukuza teknolojia ni kuleta mabadiliko ya kudumu katika matibabu ugonjwa wa kiharusi. Pia tafiti katika nyanja hii itasaidia katika zitasaidia kubuni mikakati ya kujikinga kupatwa na kiharusi miongoni mwa watu katika jamii ambao wana vihatarishi vya kiharusi.
“Dhumuni la ujio wetu hapa (MOI) ni kuanzisha ushirikiano pamoja nanyi kutoa mafunzo, tafiti na kukuzs teknolojia ya kutibu ugonjwa wa kiharusi ili kuleta mabadiliko ya kudumu katika maboresho ya tiba ya ugonjwa huo” amesema Prof. Lawton
Pia, Prof Lawton ameongeza kwa kusema kuwa Taasisi yao itahakikisha inashirikiana ipasavyo na MOI kwa kuwajengea uwezo wataalam wa taasisi hiyo ili kufikia malengo hayo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Ubongo MOI, Dkt. Lemeri Mchome amewashukuru wataalam hao kutoka Marekani kwa kuonesha nia ya kuingia makubaliano rasmi baina ya taasisi hizo mbili, ambapo kupitia makubaliano hayo, ufanisi katika matibabu ya ugonjwa wa kiharusi na kuongeza afua ya matatizo hayo.
Dkt. Lemeri amesema kupitia takwimu za tafiti za ndani ambazo hazijachapishwa, tatizo la kiharusi limechukua nafasi ya tatu ya juu kwenye magonjwa yanayoshambulia ubongo hivyo kufanya mashirikiano haya kuwa ya kimkakati.
Amesema uchaguzi wa eneo moja la ushirikiano ni mpango maalum wenye dhamira kuu ya kujielekeza kikamilifu katika kipaumbele kimoja ili kuleta mageuzi makubwa
Prof. Lawton ameambatana na Prof. Dilan Ellegala ambaye ni muasisi wa Madaktari Afrika pamoja na wataalam wengine katika misheni maalum ya Global Neurosurgery.