Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) itashirikiana na kampuni ya Joimax Spine ya Ujerumani katika upatikanaji wa vifaa tiba vya upasuaji wa mgongo kwa njia ya Matundu.
Upasuaji huo wa mgongo kwa njia ya matundu umeanzishwa na Taasisi ya MOI hapa Tanzania mwezi Machi 2025
Ushirikiano huo utafanyika kufuatia ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya akiambatana na Madaktari bingwa wabobezi wa upasuaji wa ubongo na mgongo MOI Dkt. Hamisi Shabani na Dkt. Nicephorus Rutabasibwa katika Kampuni hiyo ya Joimax nchini Ujerumani.
Dkt. Mpoki amesema makubaliano hayo itaifanya Taasisi ya MOI kuwa kituo cha weledi na mafunzo katika upasuaji wa kısasa wa mgongo kwa njia ya matundu madogo (Excellence for training in Endoscopic Spine Surgeries) baranı Afrika.