MOI, bmvss na ubalozi wa india warejesha tabasamu kwa wananchi 310 kwa kuwapatia miguu na mikono bandia bure

Na Abdallah Nassoro- MOI

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) na Taasisi ya BMVSS kwa kushirikiana na Ubalozi wa India Nchini Tanzania zimefanikiwa kurejesha tabasamu kwa wanachi 310 waliopoteza miguu na mikono kwa kuwapatia bure viungo hivyo bandia.

Mratibu wa kambi hiyo kutoka MOI Bi, Mary Chandeu amesema hayo jana Desemba, 17, 2025 wahitajji 310 kati ya walengwa 600 wamepatiwa viungo vyao saidizi bure katika kambi ya miezi miwili inayoendelea jijini Dar es Salaam.

“Ikiwa wiki tatu zimepita tangu kuanza kwa kambi hii Novemba 26, 2025 hadi leo Desemba 17, 2025 tayari wahitaji 310 wamerejeshewa tabasamu kwa kupatiwa viungo hivyo saidizi vinavyowafanya warejee katika hali zao za kawaida” amesema Bi, Chandeu na kuongeza kuwa

“Hawa ni wale waliopoteza mikono au miguu au vyote kwa pamoja, kwa ushirikiano wa MOI, BMVSS na ubalozi wa India nchini tumeweza kufanikisha uwepo wa kambi hii, ambapo wahitaji 600 wanatarajia kupatiwa viungo saidizi bure”

Amebainisha kuwa hadi sasa wahitaji zaidi ya 1,200 wamejiandikisha na idadi hiyo inaongezeka kila siku jambo ambalo amesema litaliwezesha Taifa kupata takwimu za wahitaji na kuwawezesha wataalam kupanga mipango ya kuendelea kusaidia waliobakia.

“Niwaombe watu wote wenye uhitaji wajiandikishe kupitia mfumo wa kwenye mtandao au wapige simu iliyopo kwenye matangazo yetu kwaajili ya usajili, wasisafiri kuja MOI kabla hawajapigiwa simu… Baada ya kujiandikisha wasubiri watapigiwa simu”

About the Author

You may also like these