Menejimenti yakagua hali ya utoaji huduma MOI

Na Abdallah Nassoro-MOI

Menejimenti ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) leo Septembe, 26, 2025 imefanya ukaguzi mkubwa (grand round) kuangalia hali ya utoaji huduma na miundombinu katika taasisi hiyo ili kuimarisha hali ya utoaji huduma bora kwa wananchi.

Zoezi hilo liliongozwa na Mkurugenzi wa tiba Shirikishi (DCSS) MOI Dkt. Asha Abdullah ambaye amesema katika ukaguzi huo menejimenti imebaini uwepo wa changamoto ndogondogo za miundombinu ambazo zinahitaji kufanyiwa marekebisho.

“Menejimenti imebaini uwapo wa changamoto ndogondogo za miundombinu yetu, ikiwa pamoja na kuharibika kwa mabomba ya maji na uchakavu wa baadhi ya majengo, kasoro hizi na zingine zinahitaji utatuzi wa haraka ili kuwezesha utoaji wa huduma bora endelevu kwa wananchi” amesema Dkt. Asha

Ameongeza kuwa “Ukaguzi huu unatuwezesha sisi kubaini wapi hakuko sawa ili hatua za haraka za kutatua tatizo zichukuliwe…tumekagua miundombinu na mifumo ya utoaji huduma”

About the Author

You may also like these