Mamia wajitokeza kupata matibabu mnazi mmoja

Na Abdallah Nassoro-Mnazi Mmoja

Mamia ya wakazi wa Dar es Salaam na viunga vyake wamejitokeza kupata matibabu ya bila malipo ya uchunguzi wa awali wa magonjwa yasiyoambukiza yanayotolewa na madaktari bingwa na bobezi kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.

Kaimu Meneja wa Magonjwa ya Ndani na Dawa Dkt. Deodata Matiko amesema zaidi ya wagonjwa 260 wamejitokeza kupata matibabu katika siku ya kwanza ya matibabu hayo

“Muitukio ni mkubwa, ukiacha hawa 260 tuliowasajili wapo wengine wengi tumewaomba waje kesho ili kutoka nafasi ya madaktari bingwa na bobezi kuhudumia hawa waliofika mapema” amesema Dkt. Deodata

Ameongeza kuwa “Tunaomba wateja wetu wasiwe na wasiwasi tupo hapa kuwahudumia hivyo waendelee kujitokeza kupata matibabu, hii ni fursa adhimu kwao”

Amesema huduma hizo zitaendelea kutolewa hadi jumamosi Novemba 15, 2025, hivyo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kupata vipimo vya awali, matibabu na elimu ya kujikinga.

Kwa upande wake Hadija Mrisho ambaye ni mmoja wa wagonjwa ameishukuru MOI kwa kutoka huduma hizo bure ili kuwafukia wananchi wenye kipato cha chini.

“Tunafahamu kumuona daktari bingwa ni gharama kubwa lakini hapa leo ni bure, vipimo vya awali bure, Sina cha kusema zaidi ya kuishukuru MOI”

About the Author

You may also like these