Jumuiya ya watumishi wanawake gcla watoa msaada kwa watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi MOI

Na Amani Nsello

Watumishi wanawake kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) wametoa msaada kwa kuchangia Tsh milioni 4 za upasuaji wa watoto wa 3 wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi wanaopata matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI).

Wanawake hao wametoa msaada leo Ijumaa, Machi 14, 2025 kwa watoto hao waliolazwa Wodi namba 5 katika Taasisi ya MOI.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, Mwenyekiti Kamati ya Wanawake GCLA, Veronica Chiligati amesema kuwa wao huwa wana utaratibu wa kila mwaka kutoa sadaka na matendo ya huruma sehemu mbalimbali za watu wenye uhitaji.

“Kila mwaka huwa tunatoa sadaka na kufanya matendo ya huruma kwa watu wenye uhitaji, na huwa tunafanya hivi kila tunaposherehekea Siku ya Wanawake Duniani, kwa mwaka huu tuliona tuje hapa MOI kutoa sadaka na kufanya matendo haya ya huruma”- amesema Bi. Veronica

Aidha, Bi. Veronica ameongeza kuwa mbali ya kulipia upasuaji wa watoto wa 3 wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi, wametoa pia pempasi katoni 5, Maziwa kopo 12, Wipes 3, mchele kilo 75, sukari kilo 20 na dawa za binadamu zenye thamani ya laki 721 za Kitanzania.

Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii wa MOI, Theresia Tarimo amewashukuru wanawake hao na kuwaomba waendelee kuwa na moyo huo wa kutoa kwani walezi na wazazi wa watoto hao wengi wao hutokea familia duni na hivyo kushindwa kukidhi gharama za matibabu.

About the Author

You may also like these