Fhamaz trust yachangia matibabu ya watoto 25 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi MOI

Na Erick Dilli- MOI

Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Fhamaz Trust imechangia matibabu kwa watoto 25 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi waliolazwa na wanaoendelea kupatiwa matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI).

Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo leo Jumatano Julai 16, 2025, Bi. Zarnat Datoo ambaye ameambatana na mume wake pia mmiliki mwenza wa Taasisi hiyo Bw. Jamie Satchell kutoka nchini Uingereza ameeleza gharama walizochangia za matibabu na msaada mwingine wa kibinadamu.

“Mimi na mume wangu kwa uwezo wetu tumechangia gharama ya upasuaji kiasi cha shillingi milioni 10 za Kitanzania pamoja na kiasi cha shillingi milioni 3 kwa ajili ya ununuzi wa dawa” amesema Bi. Zarnat na kuongezea

“Pamoja na kuchangia gharama hizo pia tumeweza kuwapatia kila mtoto na mzazi chakula pamoja na vifaa vya shejala kwa lengo la kuwapa tabasamu la moyo na pia kuwawezesha watoto kuendelea kujifunza hata wakiwepo hospitalini”

Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi wa MOI, Bi. Sophia Nasson ameishukuru taasisi hiyo kwa kuendelea kuwa wadau wakubwa kwa watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi wanaopatiwa matibabu katika taasisi hiyo.

About the Author

You may also like these