Na Erick Dilli- MOI
Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kwa kushirikiana na Shirika la kimataifa la AO Alliance zimetoa mafunzo ya matibabu ya mivunjiko ya Mifupa (Basic principles of fracture management) kwa madaktari wa Tanzania.
Mafunzo hayo yameanza Mei 13, 2025 katika hoteli ya protea jijini Dar es Salaam ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MOI Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya ameipongeza Shirika hilo kwa kuendeleza ushirikiano huo.
“Nipende kushukuru Shirika la AO Alliance kwa kuendeleza ushirikiano huu na kuendeleza mafunzo haya yanaofanyika kila Mwaka kwa madaktari wazawa yenye tija ya kuhakikisha matibabu bora kwa wagonjwa wanaopata mvunjiko wa Mifupa katika nchi yetu”
Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Mifupa MOI Dkt. Antony Assey amewashukuru Madaktari wazawa waliofika pamoja na waratibu wa mafunzo hayo
“Mafunzo haya huwa yanafanyika kila Mwaka na ni washukuru Madaktari wazawa pamoja na waratibu ambao mmeweza kufika kwani kwa umoja huu utasaidia sana kuhakikisha matibabu ya mivunjiko ya mifupa kwa wananchi”
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la kimataifa AO Alliance Dkt. Claude Martin JR amesema lengo la shirika ni kuhakikisha majeruhi (wagonjwa) wanapata matibabu bora katika nchi zinazoendelea barani Africa.
Mafunzo haya yameanza Mei 12, 2025 na kutamati Mei 14, 2025 na lengo ni kuhakikisha matibabu bora kwa wananchi.