MOI yatoshana nguvu na bmh shimmuta morogoro

Na Mwandishi wetu- MOROGORO

Timu ya mpira wa miguu ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imefanikiwa kupata alama moja kwa matokeo ya sare ya goli 2 – 2 dhidi ya Hospitali ya Benjamini Mkapa (BMH) kwenye mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi Tanzania (SHIMMUTA) yanayoendelea kurindima mkoani Morogoro.

Akizungumza mara baada ya mtanange huo uliochezwa leo Novemba 26, 2025  katika uwanja wa MUM uliopo Morogoro, Kocha wa timu ya MOI Max Muya amesema kuwa mchezo huo umemalizika kwa kugawana alama na timu pinzani ambapo goli limefungwa na Francesco na Binuru.

“Mchezo wa leo ulikuwa na ushindani mkali uliopelekea kutoshana kwa alama za magoli 2 kwa 2 dhidi ya timu pinzani ya hospitali ya Benjamini Mkapa na kwa sasa tunajipanga kwa mchezo ujao” amesema Muya

Timu hiyo ya MOI imecheza mechi ya pili katika hatua ya makundi kwenye  mashindano hayo ya SHIMMUTA.

About the Author

You may also like these