Watumishi MOI wapigwa msasa kanuni za kutoa huduma bora kwa wateja

Na Amani Nsello- MOI

Watumishi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wamepatiwa mafunzo maalum kuhusu utoaji wa huduma bora kwa wateja, lengo likiwa ni kuboresha mawasiliano na kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wagonjwa.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Jumatano Oktoba 08, 2025 yakiwa na malengo ya kuongeza uelewa wa watumishi kuhusu umuhimu wa maadili, uwajibikaji na utoaji wa huduma kwa viwango vinavyokidhi matarijio ya wateja.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mkufunzi kutoka Kampuni ya DIT. (DIT.Co.Ltd) Mhandisi Deograsias A. Moyo amesema

“Huduma bora kwa mteja inaanza na mtazamo chanya wa mhudumu… Mteja anapaswa kuheshimiwa, kusikilizwa na kutendewa kwa weledi bila kujali hali yake… Lengo letu ni kuhakikisha taasisi za umma zinakuwa mfano wa huduma bora zenye utu”

Kwa upande wake, Dkt. Kennedy Nchimbi , Meneja Kitengo cha Ukaguzi wa Kitabibu na Uboreshaji wa Huduma MOI (CAQA), amesema mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada endelevu za taasisi katika kuongeza ubora wa huduma.

Mshiriki wa mafunzo hayo Naseib Norroh ,Mhudumu wa Afya Mwandamizi MOI amesema mafunzo yamekuwa yenye manufaa makubwa kwa watumishi na yataongeza ufanisi.

Mafunzo hayo yamefanyika ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja ambayo hufanyika kila mwaka wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba duniani kote.

About the Author

You may also like these