Frienda of Samia wafariji watoto wenye kichwa kikubwa na mgongo wazi MOI

Na Erick Dilli- MOI

Kikundi cha umoja wa wanawake cha Friends of Samia Septemba 6, 2025 limewafariji watoto wenye ulemavu wa kichwa kikubwa na mgongo wazi wanaopata matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI).

Mwenyekiti wa kikundi hicho, Bi. Dorothy Kilavi, amesema lengo la ujio wao ni kuwafariji watoto hao pamoja na wazazi waliolazwa wodini, ikiwa ni sehemu ya kugusa maisha yao katika kipindi hiki kigumu cha matibabu.

“Kwa umoja wetu wa wanawake tunatambua Mheshimiwa Rais ana majukumu mengi ya kitaifa, hivyo tumeona kwa kile kidogo tulichobarikiwa tuje kuwafariji watoto hawa pamoja na wazazi wao. Tunaamini msaada huu utagusa sehemu kubwa katika maisha yao,” amesema Bi. Kilavi.

Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii MOI, Bi. Jalia Issa, amewashukuru Friends of Samia kwa moyo wa kipekee wa kugusa maisha ya watoto hao na kuhimiza wadau wengine kuendelea kujitokeza kusaidia safari ya matibabu ya wagonjwa hao.

Katika faraja hiyo, Friends of Samia wamekabidhi msaada wa nepi za watoto na watu wazima, maji, sabuni za kuogea pamoja na sabuni za kufulia kwa ajili ya watoto na familia zao waliolazwa hospitalini hapo.

About the Author

You may also like these