Na Erick Dilli-Arusha
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), Mhe. Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya, amepongeza ushirikiano mzuri wa utoaji huduma za afya kati ya MOI, Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya AICC, katika kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi kinachoendelea jijini Arusha.
Dkt. Mpoki ametoa pongezi hizo, Agosti 24, 2025, mara baada ya kutembelea maeneo ya utoaji huduma kwa washiriki wa kikao kazi hicho kinachofanyika katika Ukumbi wa AICC, Arusha.
“Mpangilio wa utoaji huduma umekaa vizuri, kuanzia sehemu ya viongozi kusubiria matibabu hadi hatua ya mwisho… Kinachofurahisha zaidi ni kuona kila Taasisi inashirikiana kwa namna yake kuhakikisha huduma inatolewa kwa ubora,” amesema Dkt. Mpoki.
Aidha, Daktari Bingwa wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu kutoka MOI, Dkt. zarina Shabhay, ametoa wito kwa viongozi wanaoshiriki mkutano huo kujitokeza kwa wingi kupata huduma.
Dkt. Mpoki aliambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo (JKCI), Dkt. Peter Kisenge, ambapo wote waliridhishwa na maandalizi bora na namna huduma zinavyotolewa kwa washiriki wa kikao kazi hicho.