Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imepata tuzo ya kuwa mtoa huduma bora kwa wagonjwa wanaopata ajali kazini na magonjwa yatokanayo na kazi, ambao ni wanufaika na Fao la Matibabu linalo linalotolewa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).
Tuzo hiyo ilitolewa Julai 04, 2025 katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam katika kilele cha Maadhimisho ya miaka 10 ya mfuko huo, ikiwa ni ishara ya kutambua mchango mkubwa wa MOI katika kutoa huduma bora za haraka na zenye ufanisi kwa wafanyakazi waliopatwa na madhara wakiwa kazini.
Mgeni Rasmi wa Maadhimisho hayo alikuwa Mhe. Kassim Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiambatana na Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb), Waziri wa Nchi – Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana , Ajira na Wenye Ulemavu). Ambapo Mhe. Ridhiwani aliongoza zoezi la utoaji wa tuzo.