MOI yashirikiana na taraso na rab kutoa mafunzo ya kuongeza ujuzi kwa watalaamu wa radiolojia wazawa

Na Erick Dilli – MOI

Kwa mara ya kwanza Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) imeshirikiana TARASO (Tanzania Radiology Society) na Ushirika wa RAB (Radiology Across Borders) nchini Australia kutoa mafunzo ya kuongeza ujuzi kwa wataalamu wa Radiolojia wazawa wa nchini Tanzania.

Mafunzo hayo yameanza leo juni 13, 2025 katika ukumbi wa mkutano MOI jengo jipya ambapo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt. Antony Assey amefungua Mafunzo hayo kwa kuwashukuru washiriki na kueleza mafanikio ya Idara ya Radiolojia katika Taasisi ya MOI

“kipekee niwashukuru wote kwa kuweza kufika katika Mafunzo haya natambua fani ya radiolojia hapa nchini imekuwa kwa kasi sana na naamini kwa mjumuiko huu wa watalaam kutoka Taasisi na hospitali mbalimbali tutahakikisha huduma hizi tunazitoa kwa viwango vya juu zaidi ya sasa” amesema Dkt Antony na kuongezea

“Taasisi yetu (MOI) inaendelea kukuwa katika utoaji huduma za kibingwa na kibobezi za Mifupa, Mgongo, Ubongo na Mishipa ya fahamu na mafanikio haya tunayapata kwa usaidizi mkubwa wa idara yetu ya Radiolojia”

Naye, Kaimu Meneja wa Idara ya Radiolojia MOI, Dkt. Magda Ahmed ameeleza mafunzo hayo yanafanyika kwa namna mbili ambapo kuna mafunzo ya darasani kupitia wakufunzi mbalimbali wa hapa nchini na nje ya nchi na pia mafunzo ya vitendo kwa lengo la kuhakikisha majibu na picha sahihi kwa madaktari ili kutoa huduma bora kwa wananchi.

Kwa upande wake Mtaalamu wa Rafiolojia kutoka Ushirika wa RAB ya nchini Australia Dkt. Gregory Brigg ameeleza lengo la ushirika kuanza mashirikiano haya hapa nchini.

“lengo letu ni kuhakikisha Taaluma hii ya Radiolojia inakuwa kubwa hapa Afrika na Tumeona Tanzania ukuaji ni mkubwa wa fani hii hivyo tumeona vyema kuanza mafunzo haya hapa ili kuweza kubadilishana ujuzi huu na kuweza kueneza kwa nchi zingine hapa Afrika”

Mafunzo hayo ya siku 2 yameanza leo Juni 13, 2025 na yatafikia tamati Juni 14, 2025 yakiwa na dhumuni la kubadilishana ujuzi kuhusu huduma zote muhimu zizotelewa na Idara ya Radiolojia.

About the Author

You may also like these