Na Abdallah Nassoro- MOI
Timu ya ufuatiliaji na Tathimini (M&U) ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) leo Juni 4, 2025 wameanza mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wa namna ya kufanya ufuatiliaji na tathimini ya shughuli na miradi ya Taasisi hiyo.
Mafunzo hayo yamefunguliwa na Mkurugenzi wa Fedha na Mipango Bw. Augustino Karadoga ambaye amewataka washiriki kuzingatia mafunzo hayo ili waweze kuisaidia taasisi kufikia malengo yake.
“Mafunzo haya ni muhimu kwetu timu ya ufuatiliaji na tathimini ili tuweke kupima na kusimamia utendaji kazi wetu, kuangalia miradi ufanisi wa miradi yetu” amesema Karadoga
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathimini (M&U) wa Wizara ya Afya Bw. Cloud Kumalija amesema mafunzo hayo ni nyenzo muhimu katika kufuatilia na kutathiimini utendaji wa taasisi pamoja na usimamizi wa miradi inayotekelezwa.
“Mafunzo haya yatawajengea uwezo wa kufanya ufuatiliaji na tathimini ya majukumu ya kurugenzi, idara na viteng…hii itachochea na kukuza ufanisi katika taasisi” amesema Kumalija na kuongeza kuwa
“Timu hii itawezesha taasisi kujipima utekelezaji wa malengo yake, kufanya ukaguzi wa thamani ya fedha kwenye miradi yenu”