Naibu katibu Mkuu Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo aipongeza MOI kutoa huduma za kibingwa mbeya

Na Abdallah Nassoro-Mbeya

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Methusela Ntonda ameipongeza Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kwa kutoa huduma bora za kibingwa za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu kwa washitiri wa mkutano wa 109 wa wadau wa elimu kwa umma na wakazi wa jiji la Mbeya bila malipo.

Hayo ameyabainisha leo Jumanne Februari, 18, 2025 alipotembelea banda la kutolea huduma lilipo katika eneo la City Park Garden jijini Mbeya, huku akitumia fursa hiyo kuwapa pole wagonjwa wanaondelea kupatiwa matibabu katika banda hilo.

“Niwapongeze sana kwa uamuzi huu wa kutoa huduma za matibabu ya kibingwa bure kwa washitiri na wananchi wa Mbeya, hongereni sana kwa kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi…pia nawapa pole wagonjwa na nawaombea mpone haraka” amesema Ntonda

Mapema Meneja Uhusiano wa MOI, Patrick Mvungi amemueleza Naibu Katibu Mkuu huyo kuwa Taasisi ya MOI imekua ikutekeleza kwa vitendo agizo la Serikali ya awamu ya sita la kusogeza huduma za kibingwa na kibobezi za matibabu ya mifupa, ubongo, mgongo, mishipa ya fahamu kwa wakazi wa jiji la Mbeya.

“Karibu sana mheshimiwa Naibu Katibu Mkuu, MOI tumekuja hapa kutoa huduma za kibingwa na kibobezi za mifupa, ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu na magonjwa ya ndani, huduma zetu hapa ni bure, lengo ni kusogeza huduma hizi karibu na wananchi” amesema Mvungi

Naibu Katibu Mkuu Ntondo ni mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 109 wa washitiri wa elimu kwa umma ulioandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Paramagamba Kabudi.

About the Author

You may also like these