watumishi 421 wapandishwa vyeo MOI

Na Abdallah Nassoro-MBWENI

Watumishi 421 wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wamepandishwa vyeo kwenye kada mbalimbali  katika kipindi cha Januari hadi Juni 2024.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 3, 2024 na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Orest Mushi wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa kurugenzi yake mbele ya kikao cha tano cha baraza la tano la MOI kinachoendelea katika ukumbi wa APC Bunju jijini Dar es Salaam.

“Katika kipindi hiki cha Januari hadi Juni tumeweza kupandisha vyeo wafanyakazi 421, haijawahi kutokea kwa idadi kubwa ya watumishi kupandishwa vyeo kwa wakati mmoja” amesema Mushi huku wajumbe wakimpongeza kwa kumpigia makofi

Amebainisha kuwa “Watumishi hawa ni wa kada mbalimbali, tumeongeza idadi ya wataalam washauri ambapo Medical Consultants 2 wamepatikana kupitia zoezi hilo na kufikia Consultants 6. Wapo Watumishi 16 waliopangiwa majukumu mapya (categorization) baada ya kutimiza sifa, na hawa wote walilipwa mishahara mipya kwa wakati bila kutengeneza malimbikizo( arrears”  

Kikao cha tano cha baraza la tano la wafanyakazi wa MOI kinaendelea kwa siku mbili ambapo wajumbe wanatarajiwa kujadili na kupitisha masuala mbalimbali yanayolenga kuboresha huduma katika taasisi.

About the Author

You may also like these