Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 08 Jul 2016

Posted on 08 Jul 2016

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Mpoki Ulisubisya Jana amefungua Mkutano wa kimataifa wa mafunzo kwa madaktari wa mifupa wa watoto katika ukumbi wa mikutano wa MOI ambapo mafunzo yatafanyika kwa siku 3 kuanzia tarehe 7 -9 Julai 2016. Mkutano ukiratibiwa na Serikali ya Tanzania kupitia Taasisi ya MOI pamoja na Serikali ya Uturuki kupitia ubalozi wake nchini .

Akifungua Mafunzo hayo, Dkt Mpoki alisema ni adhma ya dhati ya serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha wataalamu wa ndani wanapewa mafunzo ya mara kwa mara na kuwajengea uwezo ili waweze kutoa huduma bora kwa watanzania na kupunguza rufaa za kuwapeleka wagonjwa  nje ya nchi ambazo zinaigharimu serikali kiasi kikubwa cha fedha

Dkt Mpoki aliongeza kwamba, anawashukuru na kuwaomba wakufunzi kutoka Uturuki kuendelea na  Moyo wao wa upendo na Ubinadamu ambapo wameweza kuacha shughuli zao binafsi hususani katika kipindi hiki cha sikukuu na kuja kuwahudumia watanzania

Kwa upande mwingine Dkt Mpoki alisema anafamu fika kwamba nchi ya Uturuki ina teknolojia ya hali ya juu katika utengenezaji wa vifaa tiba, madawa na miundombinu ya hospitali ambapo tayari Wizara ya Afya imeshaanza mazungumzo na serikali ya uturuki na siku za usoni jopo la wataalamu kutoka uturuki litakuja nchini kwa ajili ya majadiliano kwani serikali ya awamu ya tano inalenga kuongeza viwanda vya ndani

Kwa upande wake Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Mh Yasemin Eralp alisema  Serikali ya Uturuki na ya  Tanzania zimekua na Ushirikiano madhubuti wa kihistoria ambao umedumu kwa muda mrefu licha ya utofauti na umbali wa kijiographia  kati ya nchi mbili na hivyo mafunzo haya lazima yaendelezwe na yawe utamuduni wa kila mwaka

Aidha, Mh Yasemin aliongeza kwamba Nchi yake ya Uturuki ina fursa nyingi hususani kwenye Nyanja za wamatibabu,vifaa tiba, miundombinu ya hospitali na viwanda vya madawa hivyo ushirikiano huo utaleta tija kwa pande zote mbili.

Aidha ,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Othman Kiloloma alisema anaishukuru Serikali ya Uturuki kupitia ubalozi wake nchini na Wizara ya Afya kwa kuwezesha mafunzo haya kufanyika kwani yatasaidia kuongeza ujuzi kwa madaktari wa Tanzania na nchi nyingine za Afrika

Kwa upande wake kiongozi wa Jopo la wakufunzi kutoka Uturuki Profesa Muharren Inan alisema ijapokuwa wamekuja kutao uzoefu wao na mafunzo kwa madaktari wa Tanzania wao pia watajifunza mambo mengi kutoka kwa madakari wa Tanzania

Katika Mafunzo hayo watoto wenye magonjwa ya mifupa watafanyiwa upasuaji,baadhi ya magonjwa hayo ni Matege, Viguu fundo, watoto wenye nyonga zilizochomoka wakati wa kuzaliwa na watoto wenye matatizo ya kuvunjikavunjika  

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano