Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 06 Jun 2016

Posted on 06 Jun 2016


Mkutano wa nne wa kimataifa wa mafunzo ya madaktari wa Mifupa duniani umefungwa leo baada ya kufanyika kwa siku nne kuanzia tarehe 31 Mei mpaka tarehe 3 Juni , katika ukumbi wa mikutano MOI pamoja na vyumba vya upasuaji MOI. Mafunzo yakiratibiwa na MOI kwa kushirikiana na Taasisi za IGOT, SIGN, OTA na Chuo kikuu cha  Calfonia San Francisco Marekani.

Mratibu wa Mafunzo hayo Dkt Kenedy Nchimbi alisema mafunzo ya mwaka huu yamehudhuriwa na madaktari kutoka zaidi ya nchi 12 Afrika ambao wamejifunza na kutoa uzoefu wao katika tathnia ya matibabu ya Mifupa. Dkt Nchimbi alisema pia mafunzo yamehudhuriwa na wakufunzi kutoka marekani na nchi nyingine za ulaya

Akifunga mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Othman Kiloloma alisema mafunzo hayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka kwa miaka 4 sasa, lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani na kuwapa mbinu mpya madaktari bingwa ili waweze kuendana na teknolojia ya matibabu duniani inayobadilika mara kwa mara

Dkt Kiloloma aliongeza kwamba mafunzo haya yamekua yakifanyika MOI kutokana na ubora wa huduma za mifupa zinazotolewa MOI ukilinganisha na hospitali nyingine katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati ambapo zaidi ya wagonjwa 5000 wametibiwa MOI kwa kutumia teknolojia ya kuweka chuma ndani ya mfupa idadi ambayo haijafikiwa na hospitali nyingine .

 Kwa maneno yake Dkt Kiloloma alisema Sisi ni kitovu cha weledi katika matibabu ya Mfupa Mrefu duniani ,ni vyema tukafanya mafunzo haya ili tuendeleze hadhi hiyo na kuwapa mafunzo madaktari wengine hapa nchini na kwingine kwote duniani”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kimataifa ya Mifupa na Ajali (IGOT) Bi Amber Caldwel alisema Taasisi yake imekuwa ikishirikiana na Chuo kikuu cha Muhimbili pamoja na Taasisi ya MOI kwa lengo la kuwajengea uwezo madaktari wa Mifupa kwote duniani kwa kutoa mafunzo kama haya ambayo yatawasaidia kutoa huduma stahiki kwa wagonjwa na kwa wakati

Bi Caldwel aliongeza kwamba anaheshimu na kutambua mchango wa Taasisi ya MOI katika jumuiya ya wataalamu wa Mifupa duniani kutokana na MOI kuwa kitovu cha weledi kwa matibabu ya Mfupa Mrefu wa paja hasa baada ya kutoa utafiti bora duniani mwaka 2015 wa matibabu ya mfupa mrefu wa paja na kuwa  idadi kubwa ya wagonjwa kuliko hospitali nyingine

Mkufunzi kutoka chuo kikuu cha Calfonia San francisco cha Marekani  Profesa Richard Oughlin  alisema kutokana na ongezeko kubwa la ajali za barabrarani duniani limepelekea mahitaji makubwa ya madaktari wa mifupa na ajali kupata mafunzo ya mara kwa mara ili kuendana na kasi hiyo inayoleta ongezeko kubwa la magonjwa ya ajali hususani katika nchi zinazoendelea kama Tanzania ambayo inakabiliwa na ongezeko kubwa la ajali za pikipiki (Bodaboda)

  

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano