Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 25 Nov 2015

Posted on 25 Nov 2015

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue ametembelea Muhimbili na kukagua utekelezaji wa Maagizo ya Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ya Uboreshaji wa utoaji huduma za Afya.

Katika ziara yake Katibu Mkuu Kiongozi ametembelea Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI na kukagua Wodi mpya zilizopo kwenye Jengo jipya la MOI (MOI Phase iii) ambazo wagonjwa wote waliokuwa wanaolala chini katika wodi za Sewahaji 17& 18 wamehamishiwa na kujiridhisha kwamba hakuna Mtanzania anapata matibabu akiwa amelala chini.

Akiwa wodini Balozi Sefue aliwajulia hali wagonjwa ambao wengi wao walionyesha sura za Matumaini kwa kufurahishwa na mazingira mapya ambayo ni mazuri ,tulivu. Wakimueleza Balozi Sefue furaha zao wagonjwa hao wameiomba serikali kuendelea na kasi hiyo hiyo ya kuboresha huduma hapa nchini

Mh Rais alitoa agizo kwamba fedha zilizokuwa zimechangwa na wahisani kwa ajili ya hafla ya kuzindua vikao vya Bunge la 11 kutumika kununulia vitanda Muhimbili (MOI) ili kuondoa adha ya  wagonjwa kulala chini ambayo imekua ni kikwazo kikubwa katika utoaji wa huduma hapa MOI


Aidha, Taasisi ya MOI imekabidhiwa jumla ya Vitanda 300, Magodoro 60,Mashuka 1,695 na viti vyenye magurudumu  vya wagonjwa 30, vitanda maalum vya wagojwa 4 kati ya 30 vinavyohitajika. Vifaa vyote vina thamani ya Shilingi Milioni 251.Manunuzi ya vifaa hivyo yamefanywa na Bohari kuu ya Madawa ya Tanzania (MSD)


Awali Katibu Mkuu kiongozi alitemebelea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kujionea namna matengenezo ya vipimo vya MRI na CT SCAN ambayo kimsingi yamefIkia hatua nzuri.

Ziara za Katibu Mkuu Kiongozi ilihitimishwa kwa Mkutano na Waandishi wa Habari uliojumuisha Katibu Mkuu wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dr Donnan Mmbando ,Mganga Mkuu wa serikali, Wakurugenzi wakuu wa MOI, MNH, JKCI, E-G-A, MSD,NHIF na watumishi wengine katika Taasisi hizo ambapo Balozi Sefue pamoja na mambo mengine amesisitiza azma ya Serikali katika kuboresha huduma za Afya hapa nchini

 

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano