Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 25 Nov 2015

Posted on 25 Nov 2015

Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametembelea Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI na kujionea hali halisi ya mazingira ya Utoaji wa huduma na kuahidi kutatua changamoto mbalimbali alizojionea.

Katika ziara yake Mh Rais alitembelea wodi za Mwaiselela namba 2, Sewahaji 17 na 18 na Kuwafariji wagonjwa ambao walifurahishwa na ziara ya Mh Rais ambayo ni ya  kushtukiza na kumuomba atatue kero mbalimbali ikiwemo ya wagonjwa kulala chini


Aidha, akiwa wodini Mh Rais amewapa pole na kuwapongeza  watumishi , wauguzi na madaktari wa MOI hususani katika wodi alizozitembelea kwa kufanya kazi katika mazingira magumu na kuahidi kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali ili kuhakikisha watanzania wanafanya kazi katika mazingira mazuri ambayo pia ni rafiki kwa afya zao

Pamoja na Mambo mengine, Mh Rais alipata fursa ya kuongea na wagonjwa ambapo walimweleza mambo mbalimbali ikiwemo tatizo la ubovu kwa mashine ya CT-SCAN na MRI ambazo zilikua na tatizo kwa muda kidogo ambapo Mh Rais aliwaahidi wagonjwa hao kwamba tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi ndani ya muda mfupi

Awali, Mh Rais alimtembelea Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za binadamu Dr Heleni Bisimba ambaye amelazwa katika Hospitali ya Agakhan Dar es Salaam baada ya kupata ajali ya gari

Hii ni ziara ya kwanza ya Mh Rais tangu aapishwe kuwa Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kukamilika kwa uchaguzi mkuu wa Tanzania oktoba mwaka huu

 

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano