Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 30 Jul 2015

Posted on 30 Jul 2015

Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Serikali ya Uturuki imeratibu mafunzo yanayohusisha mbinu mpya za kutibu mifupa ya watoto kwa madaktari wa fani ya tiba ya mifupa ya watoto wa MOI kuanzia tarehe 16/06/2015 mpaka 19/06/2015

Akizungungumza wakati wa kufungua Kongamano,Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr.Seif Rashid (MB) alisema Serikali imekua ikichukua jitihada madhubuti za kuwajengea uwezo wataalamu wake ili kuhakikisha wananchi hususani watoto wanapata huduma bora ikizingatiwa wao ni Taifa la leo na Kesho,vilevile Dkt Seif aliwaasa washiriki kuyatumia vizuri mafunzo ili yawe na tija katika kuleta mageuzi makubwa ya matibabu ya mifupa ya watoto

Mafunzo yaliendeshwa na jopo la madaktari Bingwa kutoka Chuo Kikuu cha Istanbul cha Uturuki, jopo hilo  liliongozwa na Profesa Muharrem Inan ambapo walitoa mafunzo kwa kushirikiana na Madaktari  Bingwa wa MOI, mafunzo yatafanyika kwa siku 4 siku 2 za mafunzo ya nadharia na siku 2 za mafunzo kwa vitendo ambapo zaidi ya watoto 30 walifanyiwa upasuaji

Pamoja na mambo mengine madaktari wa MOI walijifunza pia Mbinu mpya za kutibu mifupa kwa kutumia darubini maalumu (Arthroscopy) na kubadilisha viungo na mifupa  iliyoharibika kwa kuweka viungo vya bandia yaani (Arthroplasty) ili kuleta mageuzi makubwa katika matibabu ya mifupa  hapa nchini

Aidha, Mafunzo yalilenga  magonjwa ya mifupa yanayowasumbua watoto hapa Tanzania ambayo ni Mguu kifundo, matege,mivunjiko, kupishana kwa viungo ,na vilevile majeraha yanayotokana na ajali ambapo kwa sasa watoto wadogo wamekua wahanga wakubwa wa ajali hasa kwa kugongwa na vyombo vya moto kama pikipiki ambapo zaidi ya watoto 1370 waliathiriwa katika kipindi cha mwaka 2013/2014

Miongoni mwa magonjwa haya yasipotibiwa mapema yanapelekea mtoto kupata ulemavu wa kudumu, hivyo MOI inatoa wito kwa wazazi watakaopata au wenye watoto wadogo wenye matatizo ya miguu au mikono iliyopinda kuwawahisha hospitali ili watoto hao wakue vizuri na kuachana na mila potofu za kuwaficha au kutokuwapeleka hospitali

Hii ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania kwa kupitia Taasisi ya MOI kuhakikisha watoto wanapata huduma bora na kupunguza idadi ya vifo na ulemavu  unaotokana na magonjwa yanayotibika.

 

 

 

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano