MOI yatoa Mafunzo ya CORONA Kata ya Kisukuru

Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI imetoa mafunzo ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa Corona kwa wenye viti pamoja na makatibu wa mashina ya chama Cha Mapinduzi (CCM) kata yakisukuru jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendajiwa MOI amesema mafunzo hayo yamefanyika kutokana na ombi la viongozi wa Kisukuru ambao waliomba taasisi ya MOI kutoa mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo na uwelewa viongozi hao ili waka waelimishe wananchi wao.

“Tulipokea maombi ya kuja kutoa elimu hapa, tukaona tuje kwani jukumu letu ni kutibu na kuelimisha pia hivyo tumewapa elimu kuhusu ugonjwa wa Corona lakini pia tumewatoa hofu kwani kumekua na uzushi mwingi kwenye miatandao ya kijamii” Alisema Dkt Boniface

Pia Dkt Boniface amesema Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli imefanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya afya hapa nchini hivyo wananchi wasiwe na wasi wasi kwani vifaa vyote vipo na ni vya kisasa.

“Kuna uzushi mwingi kwenye mitandao kwamba hapa nchini kuna ‘VENTILATOR’ 2 habari hizo ni uzushi mtupu na nawaomba mzi puuze, pale Muhimbili, MOI, JKCI tunazo zaidi ya 99 ambazo ni za kisasa kabisa ambazo zimenunuliwa na Serikali yetu tukufu” Alisema Dkt Boniface

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wenye viti wa CCM kata ya Kisukuru Bw. Thomas Haule ameishukuru Serikali kwa jitihada kubwa za kupambana na ugonjwa wa Corona ambapo wananchi wamekua wakipata elimu na taarifa mbalimbali kuhusu ugonjwa huo.

“Nakushukuru sana Mkurugenzi kwakuja kutupa elimu, tumeelimika na elimu hii itawanufaisha wananchi wetu wote wa kata hii ya kisukuru, Pia tunashukuru kwamba Serikali yetu inawatendaji ambao wanashuka mpaka chini, hatukutegemea kama Mkurugenzi kutoka MOI angefika hapa lakini leo amekuja na ametupa elimu” Alisema Bw. Haule

Mkaziwa kata ya Kisukuru bwana Odacks Pembe ameshukuru kwa mafunzo waliyopata na kuahidi kuendelea kuchukua tahadhari ili kujiepusha na maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

“Serikali kupitia Wizara ya Afya imekuwa inafanya kazi nzuri na sisi wananchi tunashukuru sana kwani tunapata elimu, taarifa lakini pia huduma kwenye hospitali zetu ni nzuri, sisi wakazi wa Kisukuru tunaunga mkono jitihada za Mh Rais Dkt John Pombe Magufuli na tuko naye bega kwa bega” AlisemaBw. Pembe

Pia Mkufunzi kutoka MOI Bi Georgina Chirwa amewaasa wananchi wa kisukuru kufuata maelekezo yote yanayotolewa naWizara ya Afya ikiwemo kuepuka mikusanyiko, kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka na kuvaa barakoa na endapo mtu ataona dalili kupiga simu no 199