Kikao cha tatu cha baraza la nne la wafanayakazi MOI chazinduliwa

Mwenyekiti wa Baraza la wafanyakazi MOI Dkt Respicious Boniface leo amefungua Kikao cha tatu cha Baraza la nne la wafanyakazi MOI katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Baraza hilo likuhudhuriwa na Zaidi ya wajumbe 70.

Dkt Boniface amesema Baraza la wafanyakazi MOI ni chombo muhimu katika kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Taasisi  pamoja na maslahi ya wafanyakazi .

“Tumekusanyika hapa kwa lengo la kutengeneza mikakati kabambe ya kuendelea kuboresha huduma na kuifanya Taasisi yetu ya MOI kuendelea kuwa Taasisi bora inayotoa huduma bora za Mifupa, Ubongo,Mgongo na Mishipa ya Fahamu Barani Afrika” Alisema Dkt Boniface

Dkt Boniface ameishukuru Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mh Dkt John Pombe Magufuli kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika Taasisi ya MOI jambo ambalo limepelekea watanzania kupata huduma bora za mifupa, Ubongo,Mgongo na mishipa ya fahamu bila ya kwenda nje ya nchi.

Kwaupande wake Katibu wa Baraza la wafanyakazi MOI bwana Ngina Mitti amesema lengo la kikao hiki cha baraza ni kujadiliana kwa pamoja ,kutengeneza mikakati na kutafuta muarobaini ya changamoto mbalimbali zinazoikibali Taasisi.

Vikao vya Baraza hilo vinafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 05/12/2019 na tarehe 06/12/2019 ambapo wajumbe watajadiliana kwa kina na kutengeneza mikakati kabambe ya kuboresha huduma kwa watanzania.