Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 26 Oct 2016

Posted on 26 Oct 2016

Maandimisho ya siku ya Watoto wenye Vichwa vikubwa na Mgongo wazi duniani yamefanyika leo tarehe 25/10/2016 katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili MOI. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ikiwa ni “Tushirikiane kuwalea watoto na kuwafuatilia”

Akifungua maadhimisho hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Othman Kiloloma alisema Taasisi ya MOI na Serikali kwa ujumla itahakikisha kwamba watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi wanapata matibabu mazuri kwa wakati na bure.

Dkt Kiloloma amewaasa wazazi wenye watoto wenye Vichwa vikubwa na Mgongo wazi ambao hawajawapeleka watoto hospitali  Kuachana na dhana potofu ya kuwaficha majumbani au kuwapeleka kwa waganga wa kienyeji kwani matibabu yapo na yanatolewa bure na serikali

Dkt Kiloloma aliongeza kwamba Takwimu zinaonyesha zaidi ya watoto 4000 wanazaliwa hapa Tanzania kwa mwaka na watoto 500- 600 pekee ndio wanapokelewa MOI kwa mwaka hivyo ni vizuri jitihada madhubuti za kuwafuata watoto mikoani na kuwapatia matibabu kwani wengi wao wanashindwa kusafiri umbali mrefu kufuata matibabu kutokana na hali duni za kiuchumi

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wazazi wenye Vichwa vikubwa na Mgongo wazi Tanzania ‘ASBATH’ bwana Hakeem Bayakub alisema anaishukuru sana Taasisi ya MOI kwa namna ambavyo imekua ikuwahudumia watoto pamoja na kuhakikisha wanapata huduma zote za msingi ikiwemo vipimo na Upasuaji

Aidha, Bwana Bayakub aliongeza kwamba pamoja na jitihada ambazo zimefanyika bado kuna changamoto mbalimbali zinazowakabili wazazi ambazo zinakwamisha matibabu sahihi kwa watoto. Baadhi ya changamoto hizo ni imani potofu za kishirikina miongoni mwa wazazi, uelewa mdogo juu ya chanzo cha kichwa kikubwa na mgongo wazi na matibabu yake, unyanyapaa wa watoto kwa kuwaficha majumbani  na kuwatelekeza akina mama hususani pale wanapojifungua mtoto mwenye kichwa kikubwa au Mgongo wazi

Kwa upande mwingine maadhimisho yalihusisha utoaji zawadi mbalimbali kwa watoto na wazizi ambapo kampuni za kuuza na kusambaza madawa ya  Nakiete Pharmacy ilitoa mashuka pamoja na pampers kwa watoto vyenye thamani ya zaidi ya Tsh Milioni 4. Vilevile  Taasisi ya Mohamed Punjani ilitoa zawadi ya viti vya magurudumu 15 

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano