Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 22 May 2016

Posted on 22 May 2016

Wauguzi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI kupitia chama chao cha wauguzi Tangania (TANNA) wamemuenzi muasisi wa taaluma hiyo duniani Bi “Florence Nightingale” aliyezaliwa Mei 12 ,1880 kwa kuwasha taa kama ishara ya upendo kwa wagonjwa na kula kiapo cha kuendelea kutoa huduma bora kwa kusimamia maadili na taratibu za taaluma hii adhimu katika utoaji wa hudunma za Afya. Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa “Wauguzi nguvu ya mabadiliko Uboreshaji, Udhibiti wa mfumo wa Afya”

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa TANNA Tawi la MOI bwana Lucal Makusa alimweleza Mgeni rasmi kwamba pamoja na mafanikio yaliyopo MOI, wauguzi wanakabiliwa na chngamoto mbalimbali ambazo kimsingi zinapelekea mazingira magumu kiutendji. Bwana Lucas alizitaja baadhi ya changamoto ni kutokuwepo kwa uwiano kati ya wagonjwa na wauguzi, Motisha tuni, kutokupandishwa kwa madaraja kwa wauguzi kwa wakati na uhaba wa vifaa tiba  pamoja na vitendea kazi vingine katika jingo jipya la MOI (MOI Phase III)

Kwa upande wake Mgeni rasmi Dkt Othman Kiloloma  ambaye alimuwakilisha Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini MOI Bi Zakia Meghji , alisema Taasisi ya MOI inaheshimu na kuthamini mchango Mkubwa wa wauguzi katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa na kuwaomba wauguzi kuendelea na moyo huo wa uzalendo wa kufanya kazi kwa bidii kwani wamekuwa chachu ya huduma bora zinazotolewa MOI

Aidha , Dkt Kiloloma aliwahakikishia wauguzi wa MOI kwamba changamoto walizozitoa Serikali inazitambua na inazishughulikia. Akizitaja baadhi ya changamoto Dkt Kiloloma alisema suala la vifaa katika jengo jipya la MOI tayari Serikali imetenga zaidi ya billion 3 kwa ajili ya kununulia vifaa vya awamu ya kwanza huku mahitaji kamili yakiwa ni Tsh Bilion 12.

Kwa upande mwingine Dkt Kiloloma aliwahakikishia wauguzi kwamba masuala ya Motisha na stahiki za wauguzi yanakwenda kuangaliwa upya kwani viwango vilivyopo sasa ni vya zamani hivyo vitabadilishwa na suala la kupandishwa kwa madaraja tayari linafanyiwa kazi kwani ni kero ya muda mrefu hivyo utawala umeamua kulivalia njuga suala hilo

Baadhi ya washiriki waliohojiwa na mwandishi wetu walionyesha nyuso za furaha na kusema wamefurahishwa  na majibu yaliyotolewa na Mgeni rasmi kwani changamoto tajwa hapo juu zimekuwa chanzo cha utendaji duni kwa baadhi ya wauguzi hivyo utatuzi wake utaleta matokeo chanya kwa Taasisi

Maadhimisho yalianza kwa shughuli za kijamii ambapo wauguzi walitoa zawadi mbalimbal kwa watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji na Mgongo wazi waliolazwa katika wodini MOI kwa kuwapatia  zawadi mbalimbali na kuwatia moyo wazazi wenye watoto hawo. Baada ya hapo wauguzi waliandamana kuelekea kwenye  ukumbi wa mikutano MOI

 

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano