Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 20 Apr 2016

Posted on 20 Apr 2016

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh Paul Makonda leo amezindua kampeni ya  nchi nzima ya upasuaji kwa watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji na Mgongo wazi kitaalam (Hydrocephulus and Spinal Bifida) ambapo zaidi ya watoto 100 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji

Akizungumza wakati wa uzinduzi Mh Makonda ambaye amemuwakilisha Waziri wa Afya ,maendeleo ya Jamii,Jinsia wazee na watoto  Mh Ummy Mwalimu (MB) alisema anaipongeza sana Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI kwa namna ambavyo imeamua kufanya jitihada za kushirikisha sekta binafsi kuboresha huduma bila kutegemea bajeti kuu .Vilevile ameipongeza Taasisi ya GSM kwa kuamua kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha huduma za Afya kwa kudhamini kampeni hii

Aidha Mh Makonda alitoa wito kwa vijana ambao wapo mashuleni kusoma masomo ya sayansi ili wawe madaktari wa baadae ambao watawasaidia watanzania siku za usoni kwani nchi nzima ina wataalaam wa upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu tisa tu ambao wanategemewa kwa kiasi kikubwa katika tiba ya watoto wenye tatizo la vichwa kujaa maji

Kwa upande wake mwakilishi wa GSM Bwana Halfan Kiwamba alisema, Taasisi ya GSM imeguswa na hali ya watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji na mgongo wazi kwani kwa sasa hakuna kampeni yoyote ambayo imewahi kufanywa ikilenga matatizo haya ya vichwa kujaa maji na mgongo wazi ikilinganishwa na magonjwa mengine ya watoto kama usonji

Bwana Kiwamba aliongeza kwamba, Kambi hii itafanyika katika nchi nzima ambapo awamu ya kwanza itafanyika katika mikoa ya Mwanza kuanzia tarehe 27 Aprili hadi 30, 2016, Shinyanga ni Mei 2 mpaka 4, 2016 Singida Mei 6 mpaka 8, 2016 Dodoma, Mei 10 mpaka 13, 2016 na Morogoro Mei 15 mpaka 17, 2016

Aidha, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Othman Kiloloma alisema kwamba kwa sasa Takwimu zinaonyesha Zaidi ya watoto 4000 wanazaliwa kwa mwaka wakiwa na matatizo ya vichwa kujaa maji na Mgongo wazi ambapo watoto 400 hadi 700 pekee ndio wanapokelewa MOI kwa mwaka hivyo kampeni hii itasaidia kuwafikia watoto ambao wameshindwa kusafiri kuja Dar es Salaam kufuata matibabu

Dkt Kiloloma aliongeza kwamba, katika kufanikisha kampeni hii Taasisi itatoa jopo la madaktari bingwa watano wa upasuaji wa Mgongo na daktari Bingwa mmoja wa Usingizi ili kwenda kwenye mikoa mitano iliyoainishwa na kuwafanyia upasuaji watoto pamoja na kutoa mafunzo kwa madaktari wa mikoani ili waweze kuwafanyia upasuaji watoto na kuwaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu kuja MOI kufuata huduma

Taasisi ya MOI imekua ikifanya jitihada madhubuti za kuwapeleka wataalamu mikoani na kuwapatia matibabu wagonjwa katika hospitali za mikoa na wilaya ili kuwapunguzia adha ya kusafiri umbali mrefu kuja MOI ambapo mikoa ya Morogoro, Mwanza, Bukoba na Mbeya imeshanufaika  

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano