Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 19 Apr 2016

Posted on 19 Apr 2016

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Mh Ummy Mwalimu (MB) jana alifungua mkutano wa kimataifa wa tatu wa madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu katika ukumbi wa wa mikutano wa LAPF makumbusho ,Dar es Salaam.

Mkutano huo umeratibiwa na Taasisi ya MOI kwa kupitia Mratibu wa ndani Dkt Khamis Shaban kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Weill Cornell cha Marekani ambapo mafunzo yatafanyika kwa siku mbili za nadharia na siku tatu za mafunzo kwa vitendo ambapo wagonjwa ambao pengine wangepelekwa nje ya nchi watafnyiwa upasuaji

Akifungua Mkutano Mh Ummy Mwalimu (MB) alisema , imekua adhma ya dhati ya serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha madaktari wanajengewa uwezo kwa kupata mafunzo stahiki na mbinu mpya za matibabu ili kutoa huduma bora na za kisasa kwa watangania hususani kwenye eneo hili la upasuaji wa Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu

Mh Mwalimu aliongeza kwamba Serikali inatambua na kuheshimu uhusianao madhubuti uliopo kati ya Taasisi ya MOI na Chuo kikuu cha Weill Cornell cha marekani ambao umeleta matokeo chanya kwa pande zote mbili husasani ya kuwapa mafunzo kila mwaka madaktari wa Tanzania na nchi nyingine kutoka sehemu mbalimbali duniani

Akizungumzia mafunzo yatakayotolewa Mh Ummy Mwalimu alisema “Taasisi ya MOI iangalie namna ya kushusha utaalamu na mbinu hizi za upasuaji wa ubongo na mishipa ya Fahamu kwa madaktari katika hospitali za Mikoa na Wilaya kwani sio watanzania wote wanaoweza kuja kufuata huduma MOI”.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Othman Kiloloma alisema, Mafunzo haya yamekua yakifanyika kila mwaka ili kuwapa mbinu mpya madakari wa Tanzania na Nchi nyingine kutoka kote duniani kwani matibabu ni kitu kinachobadilika kila siku hivyo ni lazima kujifunza mbinu mpaya

Aidha, Dkt Kiloloma aliongeza kwamba Ongezeko kubwa la ajali za pikipiki (Bodabopda) limepelekaea ongezeko kubwa la wagonjwa wenye matatizo ya ubongo na mishipa ya fahamu hivyo ni vyema jitihada madhubuti zikachukuliwa ili kupunguza wimbi hili la ajali ambalo linagharimu maisha ya vijana wengi ambao ndio nguvu kazi ya taifa

Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Weill Cornell cha Marekani Profesa Rogers Hartl alisema yeye pamoja na jopo la wataalam kutoka nchini marekani wamefarijika kwa mara nyingine kuja Tanzania kubadilishana uzoefu na mbinu za matibabu ya Ubongo, mishipa ya fahamu na madakari wenzao wa Tanzania na wengine kutoka kwote duniani,   

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano