Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 13 Apr 2016

Posted on 13 Apr 2016

Timu ya Mpira wa Miguu ya MOI ya wafanyakazi wa zamani imetoshana nguvu kwa kutoa sare ya bila ya kufungana na timu ya wafanyakazi wapya wa MOI katika pambano la kirafiki lililofanyika katika uwanja wa Muhimbili

Pambano hilo lilifanyaika kwa lengo la kuwakaribisha wafanyakazi wapya, kufahamiana pamoja na kuimarisha kikosi cha MOI Sports club. Katika pambano hilo timu zote zilionyesha kandanda safi lenye ushindani mkali huku timu zote zikionyesha ari kubwa ya kutaka kuibuka na ushindi ijapokuwa mpaka kipenga cha mwisho kikipulizwa hakuna timu iliyokuwa imefanikiwa kuzifumania nyavu za timu pinzani kutokana na safu za ulinzi za timu zote kucheza kwa umakini mkubwa

Kikosi cha timu ya wachezaji wa zamani (Wakongwe) kiliongozwa na Nahodha msaidizi Geofrey Mhando wachezaji wengine wakiwa goli kipa Ngina Mitti, Beki wa kulia Moses Moses, beki wa kushoto Soud Mansour, beki kisiki wa katikati Venance Kalinga pamoja na Geofrey Mhando, Viungo wakiwa Haidary .C pamoja Musa Migabo, mawinga wakiwa John Ntauka,Nathani Chimoto Pamoja John Dotto ,safu ya ushambuliaji ikiongozwa na Patrick Mvungi pamoja na Humphrey Maziku  ,benchi la ufundi likiongozwa na Aidan Kipepe na daktari wa timu akiwa Elius Willium

Kwa upande mwingine, kikosi cha timu ya wafanyakazi wapya (Vijana) kiliongozwa na nahodha wake Yusuph Muhidini, goli kipa Omary Hamisi, beki wa kulia Yusuph Muhidini, beki wa kushoto Mbaraka Adam, beki wa kati Gustavo Mbunda pamoja na Frank John, viungo wakiwa Selemani Mohamed pamoja na Jonas Kabobo, mawinga wakiwa Juma. J Pamoja na Kulwa.K na safu ya ushindani ikongozwa na Swalehe Mohamedi pamoja na Yakubu, benchi la ufundi likiongozwa na Norberth Massawe pamoja na Ignace Venance

Kikosi cha MOI Sports club kimeendelea kujiimarisha ili kuendeleza historia yake ya wimbi la ushindi ambapo mwishoni mwa mwaka jana MOI ilishiriki katika Bonanza la Mashirika ya Umma na Binafsi na kunga’ra baada ya kushinda mapambano yote

Pamoja na watumishi wa MOI kuwa na ratiba ngumu za kazi hususani za kutoa huduma za afya kwa watanzania, watumishi wa MOI wamekua wakishiriki katika michezo kwa lengo la kuimarisha Afya zao pamoja na kudumisha umoja.

  

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano