Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 05 Apr 2016

Posted on 05 Apr 2016

Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii imetembelea Muhimbili na kukagua shughuli za utoaji huduma katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete

Kamati ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mh. Peter Serukamba (MB) na  Serikali ikiwakilishwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , wazee na watoto Mh .Dr Khamis Kigwangalla (MB) ilitembelea Jengo Jipya la Taasisi ya Mifupa MOI (MOI Phase III) na kujionea changamoto mbalimbali ambazo kimsingi zinatokana na Jengo kutokukamilika kwa asilimia 100% kutokana na changamoto ya kifedha

Pamoja na mambo mengine Baada ya kupewa ripoti ya kiutendaji ya Taasisi zote tatu, Mwenyekiti wa Kamati Mh. Serukamba alisema kamati imeguswa na uhaba wa bajeti inayotengwa kwa Wizara ya Afya husani kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya MOI na Taasisi ya MOYO ambayo imepelekea utoaji wa huduma kuwa mgumu na hivyo kuahidi kulifuatilia jambo hilo kwa ukaribu

Kwa upande mwingine kamati imeunga Mkono Tamko la Serikali kupitia Waziri wa Afya Mh Ummy Mwalimu (MB) ya kukemea Udhalilishaji na unyanyasaji kwa madaktari na watumishi wengine wa Afya ambapo kamati imeonyesha kukerwa na vitendo hivyo na kuwaelekeza wananchi kufuata taratibu stahiki na kuacha kujichukulia sheria mkononi

Akitoa ufafanuzi wa Mambo mbalimbali Naibu Waziri wa Afya Mh.  Dr Khamis Kigwangalla (MB) alisema kwamba Serikali imeyachukua maelekezo yote, Ushauri wa kamati kwani lengo la Serikali ni kuhakikisha watanzania wote wanapata huduma bora za Afya na si vinginevyo. Vilevile Dr Kigwangalla alisema kwamba Serikali inakemea vikali vitendo vyote vya kidhalilishaji dhidi ya Madaktari na ni vyema wananchi wakafuata taratibu za malalamiko kwenye vyombo husika na sio kuchukua sharia mkononi

Kwa upande wao wajumbe wa kamati ya maendeleo ya jamii wamepongeza kazi nzuri inayofanywa na Madaktari, wauguzi pamoja na wahudumu wengine katika sekta ya Afya ambao wanafanya kazi ngumu na nzuri katika mazingira magumu na hivyo kuiomba serikali kuingalia sekta ya Afya na Elimu kwa namna ya kipekee ili kuhakikisha watanzania wanapata huduma bora na kisasa na kupunguza wimbi kubwa la wagonjwa wanaokwenda nje ya nchi

 

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano