Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 30 Mar 2016

Posted on 30 Mar 2016

Taasisi ya GSM ya Dar es Salaam imetoa Msaada wa Shilingi Milioni 20 kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI kwa ajili ya kununulia vifaa tiba  na matibabu kwa watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na Mgongo wazi kitaalamu (  Hydrocephulus & Spinal Bifida)

Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi (Mfano) Mwakilishi wa Kampuni ya GSM Bi Shanon Kiwamba alisema GSM  imeguswa na changamoto zinazowakabili watanzania na  imeamua kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli ya kuboresha huduma za Afya hapa nchini

Bi Shanon aliongeaza kwamba pamoja na msaada wa fedha GSM ilizotoa kwa MOI, GSM itafadhili kambi za upasuaji (Surgical camps) kwa watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji na mgongo wazi katika mikoa mitano ya ya kanda ya ziwa ambapo taratibu za mwisho zinafanyika na Kambi zitaanza kufanyika mwishoni mwa mwezi wa nne ambapo tarehe itatolewa baadae

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Othman Kiloloma,alisema anaishukuru Taasisi ya GSM  kwa kuguswa na hali za watanzania hususani watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji na mgongo wazi ambao kimsingi wanahitaji kufarijiwa na watanzania wenzao.  Dkt kiloloma aliongeza kwamba GSM imefanya maamuzi sahihi ya kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano za kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma bora za afya kwa wakati muafaka

Aidha, Dkt Kiloloma alisema kwamba fedha zilizotolewa na GSM zitatumika kama ilivyoelekezwa , Vilevile MOI iko tayari kutoka wataalamu kwenda Mikoani kuwafanyia upasuaji watoto katika hususani mikoa ya kanda ya ziwa kwa kutumia vifaa vya MOI ili kuwapunguzia adha wagonjwa kusafiri kuja Dar es Salaam kufuata huduma

Taasisi ya MOI imekua ikichukua jitihada madhubuti za kuhakikisha watanzania hususani watoto wenye  vichwa vikubwa na Mgongo wazi wanapata huduma Bora pale walipo ambapo Taasisi imekua ikipeleka wataalamu mikoani kwa ufadhili wa wadau mbalimbali na kuwafanyia upasuaji watoto ambapo Mikoa ya Morogoro, Bukoba na Mwanza imeshanufaika

Takwimu zinaonyesha hapa Tanzania watoto zaidi ya 5000 kwa mwaka wanazaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi ambapo watoto 400-500 pekee ndio wanapokelewa hapa MOI kwa mwaka

  

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano