Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 29 Feb 2016

Posted on 29 Feb 2016

Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya MOI Bi Zakia Meghji amezindua vikao vya Baraza la Tatu la Wafanyakazi wa MOI jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa NIMR. Mkutano ukihudhuriwa na wajumbe zaidi ya 70 kutoka katika idara mbalimbali ambapo vikao vitafanyika kwa siku 3

Akizungumza wakati wa kuzindua vikao vya Baraza hilo, Bi Meghji aliwahawahakikishia wajumbe kwamba Bodi ya wadhamini ya MOI pamoja na menijimenti ya MOI zinafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha changamoto zinazoikabili Taasisi ya MOI kwa sasa zinatatuliwa ili kuhakikisha kwamba watanzania wanapata huduma bora katika jengo Jipya la MOI

Aidha,Bi Meghji amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa jitihada alizochukua za kuboresha huduma za Afya hapa nchini hususani kuondoa changamoto ya wagonjwa kulala chini ambayo imekua sugu kwa siku nyingi

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Othman Kiloloma alisema kwamba kwa sasa Taasisi ya MOI kwenye mageuzi makubwa katika kutoa huduma kutokana na wagonjwa wote kuhamishiwa kwenye jengo Jipya la kisasa la MOI (MOI Phase III) na vikao vya Baraza hilo vitalenga mradi huo ili kuhakikisha Matarajio ya watanzania ya kupata huduma bora za kisasa yanafikiwa

Pamoja na Mambo mengine, Bi Zakia Meghji aliwakabidhi vyeti na zawadi Wafanyakazi bora wa Mwaka wa fedha uliopita ambapo Bi Mkaseko Mtema akiibuka kidedea na kupata zawadi ya Shilingi Milioni 1 na nusu.

Vikao vya Baraza la 3 la wafanyakazi wa MOI vilifungwa siku ya ijuma tarehe 26/2/2016 na Mwenyekiti wa Baraza hilo Dkt Othman Kiloloma ambaye aliwapongeza wajumbe wote kwa namna ambavyo wamekua wakitoa hoja mbalimbali ambazo zililenga kuboresha utoaji wa huduma kwa watanzania .Aidha alwapongeza katibu wa Baraza hilo Dkt Clement Mugisha pamoja na Msaidizi wake Bi Eveline Machumu na sekretarieti kwa kazi nzuri ya kuratibu Baraza hilo

Taasisi ya MOI imekua ikitekeleza dhana ya utawala bora na uwazi na maamuzi shirikishi (Good governance, Transparence and Participatory decision making) ambapo wafanyakazi wa MOI kupitia wawakilishi wao katika baraza la wafanyakazi wamekua wakifanya maamuzi kwa kushirikiana na utawala katika vikao vya mabaraza ya wafanyakazi  

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano