Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 24 Jan 2016

Posted on 24 Jan 2016

Kampuni ya Mafuta ya Dalbit Petroleum imeunga mkono jitihada za serikali za kuboresha huduma za afya hapa nchini kwa kutoa Vitanda 27 na magodoro  vyenye thamani ya dola za kimarekani 7,500 (Milioni 16) kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI kwenye wodi ya watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi

Vitanda hivyo  vimekabidhiwa na  Mkurugenzi Mkuu wa Dalbit Margaret Mbaka kwa Mganga mkuu wa Serikali profesa Muhammad Kambi ambaye aliwakilisha wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii

Akizungumza wakati wa kukabidhi vitanda hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Dalbit Margaret Mbaka alisema, Dalbit imekua ikitenga fedha kutoka kwenye faida yake ya mwaka ili kusaidia mambo mbalimbali ya kijamii hususani Afya ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii (CSR) na kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano za kuboresha huduma za afya hapa nchini

Kwa upande wake  Mganga Mkuu wa serikali Profesa Kambi alitoa pongezi na shukrani kwa kampuni ya Dalbit kwa kuamua kushirikiana na serikali katika kuboresha huduma za Afya hapa nchini ambapo pia alishauri ushirikiano wa MOI na Dalbit uendelee ili kuleta manufaa zaidi kwa watanzania . Vile vile aliwaasa watumishi MOI kutumia vitanda hivyo vizuri kwa manufaa ya watanzania wote

Aidha, Akitoa neno la Shukrani kwa niaba ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI,Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi  Flora Kimaro alitoa shukrani za dhati kwa kampuni ya Dalbit kwa namna ambavyo imeguswa na kuamua kushirikiana na Serikali katika kuboresha huduma za Afya na kuahidi kuvitumia vitanda hivyo kwa manufaa ya watanzania wote ambapo pia alitoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano wa Dalbit kwa kujitokeza  kuunga mkono jitihada za serikali

Vitanda hivyo vimetolewa pamoja na runinga moja katiaka wodi za watoto katika jengo jipya la MOI (MOI Phase III) ghorofa ya tano (Wing A) ambapo watoto wenye vichwa vikubwa na Mgongo wazi watahamishiwa . 

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano