Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 16 Dec 2015

Posted on 16 Dec 2015

Maadhimisho ya Siku ya watoto wenye matatizo ya Vichwa kujaa maji na Mgongo wazi duniani yamefanyika  ambapo wazazi  100 na wadau mbalimbali walishiriki . Huku takwimu zikionyesha kwamba zaidi ya Watoto 4800 wanazaliwa na matatizo hayo kwa mwaka hapa Tanzania ambapo kila mwaka watoto 400 pekee ndio wanapokelewa katika Taasisi ya MOI kama wagonjwa wapya

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Bwana Jumaa Almasi ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa MOI alisema ni vyema kusherehekea siku hiyo adhimu kwa sababu watoto hawa ambao leo ni wagonjwa wakipatiwa matibabu sahihi wanaweza kuwa viongozi wakubwa na kuliletea taifa maendeleo

Maadhimisho yalianza kwa maandamano ya amani yaliyoanzia katika ofisi za chama cha wazazi wenye matatizo hayo (ASBATH) na kufikia tamati katika wodi walizolazwa watoto wenye matatizo hayo huku washiriki wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wa kauli mbiu ya mwaka huu inayosema ‘‘Kwa pamoja tuzuie Ulemavu wa Kuzaliwa’’

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha wazazi wenye watoto hao (ASBATH) Bwana Hakeem Bayakub aliushukuru uongozi wa MOI kwa namna ambavyo umekua ukichukua jitihada madhubuti kuhakikisha watoto wanapata Tiba stahiki na  ushirikiano mkubwa kwa chama chao. Vilevile Bwana Hakeem aliwaomba wafadhili ambao wamekua wakiwasaidia watoto hao kuendelea na Moyo huo huo na kuomba wafadhili wengine kujitokeza ili kukisaidia chama chao kutekeleza majukumu yake ipasavyo

Aidha ,Mwenyekiti wa kamati ya wafanyabiashara wa kariakoo mtaa wa Raha square  na Mhonda Bwana Ludovick Mmasi alisema kwamba wameshiriki katika maadhimisho hayo kwani wameguswa na hali za watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji na mgongo wazi na kuamua kuunganisha umoja wao ili kuwasaidia watoto hao .Umoja huo uliwapatia watoto zawadi mbalimbali ambazo ni vyakula, sabuni ,pampas, mafuta pamoja na kujitolea damu

Pamoja na mambo mengine,vipo vyanzo vingi vya ugonjwa wa vichwa kujaa maji na mgongo wazi kitaalamu (Hydrocephulus and Spinal Bifida) lakini sababu kuu ikitajwa kuwa ukosefu wa virutubisho vya folic acid kwa Mama wakati wa ujauzito na kupelekea kupata watoto ambao njia zao za kuingiza maji na kutoa maji yanayozunguka ubongo kuziba na kusababisha kichwa kuongezeka ukubwa au uti wa mgongo kutokufunga na  kusababisha uvimbe mgongoni.

 

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano