Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 15 Dec 2015

Posted on 15 Dec 2015

TAARIFA

Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya fahamu (MOI) kwa kushirikiana na Shirika la Friends of Children with Cancer Tanzania (FOCC) imeandaa kambi maalum ya matibabu na upasuaji wa watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji na mgongo wazi (Hydrocephalus and Spinal Bifida)

Kambi itafanyika siku ya Jumapili tarehe 20-12-2015 katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) ambapo watoto watapatiwa matibabu, Ushauri na upasuaji bure.

Aidha,Wazazi wenye watoto wenye matatizo hayo wanatakiwa kuwaleta watoto siku ya Jumatano tarehe 16-12-2015 na Ijumaa tarehe 18-12-2015 asubuhi saa 1:30 kwa ajili ya uchunguzi/ usajili . Wale watakaolazwa wodini tu ndio watafanyiwa upasuaji.

Imetolewa na

Dr Samweli Swai

Kaimu ,Mkurugenzi wa Tiba

 

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano