Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)
Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology
Date : 07 Sep 2015
Posted on 07 Sep 2015
Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI imeshiriki katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyofanyika kuanzia tarehe 24-28 August 2015 katika viwanja vya mnazi mmoja Dar es Salaam,Maadhimisho hayo yalifunguliwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam CP Suleiman Kova
Maadhimisho hayo yalishirikisha Taasisi mbalimbali za Umma na binafsi pamoja na makundi mbalimbali ya kijamii lengo ikiwa ni kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara ili kupunguza ajali, vifo na Ulemavu, Kauli Mbiu ya Maadhimisho hayo ikiwa ni “Endesha salama, okoa maisha”,
MOI imekua ikishiriki katika maadhimisho haya kila mwaka kutokana na kuwa mdau mkubwa wa ajali za barabarani kutokana na kupokea idadi kubwa ya majeruhi wa ajali za barabarani katika ukanda huu wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani ya Pwani na Morogoro
Aidha, wataalamu wa MOI walipata fursa ya kutoa elimu kwa waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda , wanafunzi na umma wa watanzania ambao walishiriki katika maadhimisho kuhusiana na madhara yatokanayo na ajali
Pamoja na mambo mengine, wajumbe wa Kamati ya usalama wa barabarani ikiongozwa na Mwenyekiti wake bwana Elifadhili Mgonja ilitembelea majeruhi waliolazwa MOI Sewahaji wodi 17,18 na Mwaisela 2 na kuwapatia zawadi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuwafariji na kuwatia moyo
Akitoa salamu za ukaribisho kwa kamati, Afisa uhusiano wa MOI bwana Patrick Mvungi aliwaeleza wajumbe kwamba Taasisi imefarijika na namna ambavyo kamati imeguswa na kuamua kuja kuwaona majeruhi wa ajali, bwana Mvungi aliongeza kwamba MOI inapokea idadi kubwa wa ajali hususani wanaotokana na ajali za pikipiki ambao kwa sasa ni aslimia 53% ya wagonjwa wote wanaopokelewa
Taasisi ya MOI imekuwa ikishirikiana na Jeshi la polisi ili kuhakikisha majeruhi wanapata huduma stahiki kwa wakati ,vilevile kupeana taarifa zinazoweza kusaidia kupunguza matukio ya ajali za barabarani ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusiana na madhara yatokanayo na ajali.
Jumatatu - Ijumaa
: 06:00 Asu - 07:00 Asu
: 06:00 AM - 07:00 AM
Jmosi / Jpili & Sikukuu
: 06:00 AM - 07:00 AM
: 07:00 PM - 08:00 PM
: 06:00 AM - 07:00 AM
Hati Miliki © 2014 Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI). Haki Zote Zimehifadhiwa