Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 30 Jul 2015

Posted on 30 Jul 2015

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mh Zakia H.Meghji (MB) kuwa mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya MOI, uteuzi huu umetokana na bodi ya wadhamini iliyokuwepo kuisha muda wake, uteuzi huo utadumu kwa miaka 3

Aidha, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii ,Dkt Seif S.Rashid (MB) amewateua Dkt Sijenunu Aaron, Prof.Bakari Lembariti,Bi J.A Safe na Dkt  Eric  A. Aris kuwa wajumbe wa bodi hiyo ambapo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Othman Kiloloma ni katibu wa Bodi hiyo

Bodi hiyo imeanza vikao rasmi tarehe 27/07/2015 katika ukumbi wa Mikutano wa MOI ambapo mambo mbalimbali yalijadiliwa kwa kina ambayo yalilenga Changamoto mbalimbali zinazoikabili Taasisi kwa sasa lengo kuu ikiwa ni kuimarisha utoaji wa huduma za afya hapa nchini.

Mh Meghi aliwaeleza wajumbe kwamba Anafahamu fika kwamba kazi iliyoko mbeleni ni ngumu ,inayohitaji ufanisi na Utashi mkubwa katika kutafuta majawabu ya changamoto zinazoikabili Taasisi ikizingatiwa kwamba watanzania wana imani kubwa na huduma za MOI hivyo ni vyema imani hiyo ikaimarishwa kwa kuendelea kutoa huduma bora

Baada ya Vikao vya Bodi kufunguliwa ,wajumbe walipata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya MOI ambayo ni Chumba cha Mitambo ,Idara ya Mazoezi Tiba (Fiziotherapia), karakana ya kutengeneza Viungo bandia, Vyumba vya wagonjwa Mahututi,vyumba vya upasuaji, wodi za wagonjwa na ziara ilihitimishwa kwa kutembelea Mradi wa Jengo jipya (MOI Phase III) ambao umekamilika kwa Asilimia 95% .Mradi huo unategemewa kuanza kazi mwaka huu.

Kwa upande wao wajumbe wa Bodi walipongeza jitihada ambazo zimefanywa na menejimenti ya MOI za kubuni vyanzo vipya vya mapato,kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato.Vilevile wajumbe waliguswa na Msongamano wa wagonjwa wodini na kuahidi kushirikiana na Mwenyekiti ili kuhakikisha Jengo jipya la MOI linafunguliwa mapema iwezekanavyo

Akihitimisha kikao cha bodi Mh Meghji aliushukuru uongozi wa Taasisi kwa jitihada zote ambazo zimefanyika ili kuhakikisha MOI inaendelea kutoa huduma bila kuwa na bodi kwa zaidi ya mwaka mmoja na kuahidi kutoa ushirikiano wa dhati ili kudumisha jitihaza hizo,vilevile kuendeleza mazuri yote yaliyofanywa na Bodi iliyopita.

 

 

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano