Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Mifupa Muhimbili(MOI)

Offering Services in Orthopaedics, Neurosurgery, and Traumatology

Habari na Matukio

Date : 30 Jul 2015

Posted on 30 Jul 2015

Jumuiya ya Kimataifa imemuenzi Muasisi wa Taifa la Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela Katika siku yake ya kuzaliwa inayoadhimishwa tarehe 18 July kila mwaka kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii katika wodi ya Watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji , Mgongo wazi (Hydrocephulus and Spinal Bifida) na Mifupa waliolazwa Wodi A hapa MOI

Shughuli hizo zilihusisha kusafisha mazingira ya nje na ndani ya Wodi kwa kufyeka,kufagia, kusafisha Madirisha,kusafisha Kuta, kufua,kupika,kusafisha maliwato na kubwa zaidi kuwapatia Watoto Zawadi mbalimbali ambazo zimetolewa na wadau mbalimbali wa Afya,zawadi hizo zilikabidhiwa kwa wawakilishi wa wazazi  na Balozi wa Afrika kusini Nchini Tanzania bwana Thami Mseleku pamoja na Mwakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa bwana Alvaro Rodriguez

Awali wakati wa kuwakaribisha wageni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt.Othman Kiloloma alisema Jamii nzima ya MOI imefarijika na uamuzi wa Jamii ya kimataifa kuamua kuja kuadhimisha siku ya Mandela MOI Kitendo ambacho kinaakisi maisha halisi ya Mzee Nelson Mandela aliyetumia muda wake mwingi kupigania haki za wanyonge hususani watoto na wagonjwa

Aidha ,akitoa hotuba yake Balozi wa Afrika Kusini Nchini Tanzania Bwana Thami Mseleku alisema Mandela alitumia miaka 67 katika kupigania haki za wanyonge hivyo ni vyema kumuenzi kwa kufanya shughuli mbalimbali kwa muda wa dakika 67 wodini, Vilevile bwana Mseleku alisema Maadhimisho ya Mandela yanatakiwa yawe kila siku kwa kuenzi matendo yake mema ya kutetea wanyonge na kuahidi kuendelea kuwasaidia watoto wenye matatizo ya vichwa kujaa maji kwani wanahitaji upendo wa dhati kama watoto wengine

Akitoa neon la Shukrani kwa niaba ya Jumuiya ya MOI Meneja Ustawi wa Jamii na Uhusiano Bwana Jumaa Almasi alisema kwa wafanyakazi wa MOI kila siku ni ‘Mandela Day’’ kwani wanaendelea kutoa huduma , kuwafariji na kuonyesha Upendo kwa wagonjwa, Vilevile aliwashukuru wote ambao wameguswa kwa kutoa zawadi kwa wagonjwa ambazo zitawatia moyo na kuwafariji

Maadhimisho yalishirikisha makundi mbalimbali ya kijamii ambayo ni uwakilishi kutoka Umoja wa Mataifa, Vodacom Tanzania, Ubalozi wa Afrika Kusini, wanafunzi kutoka Shule mbalimbali,watu binafsi walioguswa na Harakati na Maisha ya Mzee Mandela ya kupigania haki za wanyoge na wawakilishi wa jamii ya wafanyakazi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI.

 

Book Online

Saa za Kuona Wagonjwa

Jumatatu - Ijumaa

: 06:00 Asu - 07:00 Asu

: 06:00 AM - 07:00 AM

Jmosi / Jpili & Sikukuu

: 06:00 AM - 07:00 AM

: 07:00 PM - 08:00 PM

: 06:00 AM - 07:00 AM

Miradi & Ushirikiano